
MASHAIRI FESTIVALs
October 4 @ 9:00 am - 4:00 pm

Funga Safari! Fika Uwasilishe Ushairi Wako! 🎤🇹🇿
📯Wito kwa Washairi Wenye Umri wa Miaka 19-30!
Mashairi Festival inakuletea fursa KUBWA zaidi ya kukuza kipaji chako cha ushairi! Tunatafuta Washairi 20 mahiri (kwa mujibu wa mashindano ya wazi) watakaopata mafunzo maalum na kupanda jukwaa kuu katika Tamasha la Kimataifa la Sanaa Bagamoyo (TASUBA) mnamo Novemba 2025. Hii ndiyo nafasi yako ya kuwa Mshairi Kiongozi wa Mabadiliko!
📯TAHADHARI MUHIMU:
HATUHITAJI MAOMBI MTANDAONI! Ili kushiriki, unachotakiwa kufanya ni KUFIKA MOJA KWA MOJA kwenye maeneo ya usaili ukiwa na shairi lako LOLOTE. Njoo, wasilisha, na uonyeshe ubunifu wako!
📯Kwanini Ushiriki???
Fursa ya Kitaifa: Tumia ushairi kama chombo cha utetezi wa kijamii na kujitambulisha kwenye jukwaa kubwa.
Andika Historia: Fanya usaili na upate nafasi ya kuunganisha mila za ushairi wa Kiswahili na mitindo ya kisasa.
📯Usikose! Maneno Yako Yana Nguvu!
#MashairiFestival
#Usaili
#UshairiTanzania
#FikaUwasilishe
#SautiTek
#TaSUBa
#FursaKubwa