MUVI KALI
March 10 @ 7:30 pm
Free
Muvi Kali at Goethe-Institut
Next Tuesday, join us for a screening of Kichaa Kichizi, a gripping Tanzanian gang-action film by director Novatus Mugurusi.
Set against the intense backdrop of Dar es Salaam’s urban landscape, the film follows a woman on a relentless search for justice after surviving a brutal assault. Her journey unfolds through a tense and powerful narrative that explores vengeance, survival, and the blurred lines between justice and morality.
Known for his strong urban storytelling, Mugurusi brings over 15 years of filmmaking experience to the screen, delivering a fast-paced and visually striking film that captures the raw energy of the city while provoking conversation about violence, resilience, and accountability.
Join us for another Muvi Kali evening celebrating bold storytelling in Tanzanian cinema.
📅 Tuesday, 10 March 2026 🚪 Doors open: 6:30 PM 🎬 Film starts: 7:30 PM 📍 Goethe-Institut Dar es Salaam
#MuviKali #TanzanianCinema #GoetheDar #FilmScreening #DarEsSalaamEvents
***
🎬 Muvi Kali katika Goethe-Institut
Jumanne ijayo tunakukaribisha kwenye onyesho la filamu Kichaa Kichizi, filamu ya gang-action kutoka kwa mwongozaji Novatus Mugurusi.
Filamu hii imejikita katika mazingira ya jiji la Dar es Salaam na inasimulia safari ya mwanamke anayetafuta haki baada ya kupitia tukio la kikatili. Hadithi hii yenye msisimko mkubwa inachunguza masuala ya haki, kulipiza kisasi, na mipaka inayotenganisha maadili na uhalisia wa maisha.
Akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika utengenezaji wa filamu, Mugurusi anaonyesha ustadi wake wa kusimulia hadithi za mijini kupitia filamu yenye kasi, mvuto wa kimuonekano, na inayochochea mjadala kuhusu ukatili, uthabiti, na uwajibikaji katika jamii.
Jiunge nasi kwa jioni nyingine ya Muvi Kali inayosherehekea ubunifu na nguvu ya sinema ya Tanzania.
📅 Jumanne, 10 Machi 2026 🚪 Milango hufunguliwa: Saa 12:30 jioni 🎬 Filamu inaanza: Saa 1:30 usiku 📍 Goethe-Institut Dar es Salaam